1 Thessalonians 4:14-17

14 aKwa kuwa tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka, na kwa hivyo, Mungu kwa njia ya Isa atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini ndani yake. 15 bKulingana na neno la Bwana mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia waliolala mauti. 16 cKwa maana Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza. 17 dBaada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Copyright information for SwhKC